Matangazo

ZILIZO KUPITA HIZI HAPA.

Bongo Flava ni sawa na mtoto anayelelewa na mama peke yake

LEO NI LEO MAN U NA CHELSEA

Views:
Video Information
MOURINHO AZIDISHA PRESHA KUISAKAMA MAN UNITED!
>>MAN UNITED WAMPUUZA, WAMPASHA KUPAYUKA HAKUMSAIDII MECHI HII!
Meneja wa Chelsea Jose Mourinho amezidi kuisakama Manchester United ambayo leo Usiku wanaifata huko Old Trafford kucheza nayo Mechi ya Ligi Kuu England kwa kudai kuwa ni makosa ya David Moyes yaliyomfanya Straika wao Wayne Rooney akose furaha na kutaka kuihama Man United.

DONDOO MUHIMU:
-Msimu wa 2012/13: Man United iliifunga Chelsea 3-2 huko Stamford Bridge na Chelsea kuifunga Man United 1-0 Uwanjani Old Trafford katika Mechi ambayo haikuwa na umuhimu kwa Man United kwani tayari walikuwa washatwaa Ubingwa.

Chelsea wameshatoa Ofa mbili kwa Man United ili kutaka kumnunua Rooney na zote kukakataliwa huku Man United ikisisitiza Mchezaji huyo hauzwi.

NINI WAMESEMA??
MOURINHO KUHUSU MAN UNITED: "Nimefungwa. Nimeshinda. Nimetoka Sare. Nimewatoa CHAMPIONZ LIGI. Wamenitoa CHAMPIONZ LIGI. Nina kila kitu dhidi yao. Labda nimeshinda Mechi nyingi zaidi yao. Labda. Lakini Siku zote nafurahia kucheza na Man United!"

DAVID MOYES KUHUSU MECHI YAKE YA KWANZA OLD TRAFFORD: "Kuna vitu vingi nilikuwa nikivingoja kwa hamu: kuiongoza Timu kwenda kwenye Ziara, kuwaongoza Uwanjani Wembley! Lakini kuiongoza Timu kwa mara ya kwanza kukanyaga Old Trafford, tena dhidi ya Chelsea, ni kitu kinachonisisimua na kunipa motisha! "

MAN_UNITED_v_CHELSEA-VIKOSI26AUGHuku Timu hizo zikitarajiwa kupambana leo Usiku Uwanjani Old Trafford na Moyes kudokeza kuwa Rooney atacheza Mechi ya leo baada ya kuwa fiti, Mourinho amekuwa akibatuka maneno ya kusudi kabisa yenye nia ya kuleta mchecheto na kuwabomoa kiakili Man United.
Akijaribu kuisakama Man United kwa kumtumia Rooney, Mourinho alitamka: “Ni Moyes ndie amesababisha Rooney kukosa furaha na kutaka kuhama aliposema Rooney ni chaguo la pili nyuma ya Robin van Persie!”
Lakini Wanahabari walipomjulisha Mourinho kuwa atakiona cha moto akiingia Old Trafford kwa kupokelewa na kelele na mashambulizi ya Washabiki, Mourinho alisema: “Wao wanipinge mimi? Sio mimi niliesema Rooney ni chaguo la pili! Sisi tunataka kumchukua Mchezaji ambae wao wanamwona chaguo la pili. Sisi hatumfuati Van Persie!  Wasinilaumu mimi. ”
Hata hivyo, Kambi ya Man United imekuwa ikipuuza maneno ya Maurinho ambayo kwao wanayachukulia kama ni mbinu ya makusudi ya kutaka kuibomoa kiakili Man United.
Wakijua hilo, Beki Veterani, Rio Ferdinand, ameeleza kuwa Jose Mourinho ataongeza chachu ya mpambano wa Jumatatu kati ya Man United na Chelsea.
Rio amesema: “Yeye ana mvuto kwa Wanahabari. Akiwepo Magazeti yanapata habari kwa Wasomaji wao. Kama hilo litawasaidia kufika tulikofika sisi Mabingwa Msimu uliopita tusubiri tuone. Hilo halimsaidiii lolote kwa Mechi hii!!”
Uso kwa Uso
-Man United na Chelsea zimekutana kwenye Mechi rasmi za Mashindano mara 161 na Man United kushinda Mechi 68, Chelsea 45 na Sare 48.
-Katika Mechi 42 za Ligi Kuu walizokutana Man United wameshinda mara 13, Chelsea 14 na Sare ni 15 na kati ya hizo ni 3 tu ndio zilikuwa 0-0 draws (Aprili 1995; Desemba 1998; Mei 20
Similar Videos