Video Information
![]() |
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao
cha NEC, mjini Dodoma leo mchana. Kushoto ni Katibu Mkuu
wa CCM Abdulrahman Kinana.
|
Kikao hicho pia kimeridhia, uteuzi
wa Makatibu wateule wapya wa Jumuia za CCM, za Umoja wa Vijana wa CCM
(UVCCM), Jumuia ya Wazazi na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT).
Katika uteuzi huo mapendekezo hayo
yaliyofanywa na Kamati Kuu ya CCM, na kuridhiwa na NEC, kwa upande wa
Umoja wa Vijana wa CCM ameteuliwa aliyekuwa Kaimu Katibu wa CCM mkoa wa
Morogoro, Sixtus Mapunda na kwa upande wa Jumuia ya Wazazi ni Mjumbe wa
NEC kutoka Pemba, Seif Shabani Mohamed, huku kwa upande wa UWT akiachwa
Katibu Mkuu wa sasa, Amina Makilagi.
Mapunda atachukua nafasi iliyokuwa
imneshikiwa na Martine Shigela ambaye ameongoza UVCCM kwa miaka mitano
sasa, na Seif Shabani Mohammed kutoka Pemba akichukua nafasi iliyokuwa
ikishikiliwa na Hamis Suleiman Dadi ambaye pia amekuwa katika wadhifa
kwa miaka mitano sasa.
Pia, NEC imeridhia mapendekezo ya
Kamati Kuu kwa ajili ya kuziba nafasi Makatibu wa CCM wa mikoa mitatu
ya Morogoro, Kaskazini Pemba na Geita ambayo kwa mujibu wa maelezo
yaliyotolewa imekuwa wazi kwa muda mrefu sasa kutrokana na sababu
mbalimbali ikiwemo kifo.
Kufuatia mapendekezo hayo ya
Kamati Kuu, ambayo yameridhiwa na NEC, walioteuliwa na mikoa yao ikiwa
kwenye mabano ni Msaidizi Kitengo cha Uchaguzi, CCM Ofisi Ndogo ya
Makao Makuu ya CCM, Romuli Rojas John (Morogoro), aliyekuwa Katibu wa
wilaya ya Mkinga, Kassim Mabrouk Mbarak (Kaskazini Pemba) na aliyekuwa
Katibu wa CCM Igunga, Mary Maziku (Geita).
Kuhusu sakata la madiwani wa
Bukoba mjini, CCM imesema suala hilo, linaendelea kushughulikiwa ambapo
baada ya kikao hicho cha NEC, Kamati kuu iliendelea kukutana na viongozi
wa wilaya ya Bukoba, Mwenyekiti wa CCM na Katibu wa wilaya hiyo.
Mapema kabla ya kikao cha NEC,
Kamati Kuu ilikutana na Mbunge wa Bukoba mjini Khamis Kagasheki na Meya
wa Manispaa ya Bukoba mjini na kuwahoji, wakati jana Kamati Kuu
ilikutana na Mwenyekiti na Katibu wa CCM mkoa wa Kagera.
Mwenyekiti
wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao cha NEC, leo Agosti 26,
2013 mjini Dodoma. Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitoa utangulizi kabla ya
Mwenyekiti wa CCm Rais Jakaya Kikwete (kushoto) kufungua kikao cha NEC,
Agosti 26, 2013
Baadhi ya wajumbe wa NEC,
ukumbini. Kulia mstari wa mbele ni Mjumbe wa Kamati ya Ushauri ya
Viongozi wastaafu wa CCM, John Malecela ambaye ni mwalikwa kwenye kikao
hicho.
Mjumbe wa NEC, Mama Salma Kikwete
akiteta jambo na Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha, Zakiah Meghji kabla ya
kikao cha NEC kuanza, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.
Mjumbe wa NEC, Dk. Fenela
Mkangala na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose
Migiro wakijadili jambo kabla ya kikao cha NEC kuanza leo Agosti 26,
2013, Makamo Makuu ya CCM mjini Dodoma.
Wajumbe
wa NEC kutoka Pemba wakiwa nje ya ukumbi kabla ya kikao kuanza. Kutoka
Kushoto ni Hamadi Bakari Ali, Mwinyi Fakih Hassan, Ali Issa Ali, Masoud
Mohammed Abdallah, Seif Shaaban Mohammed na Mussa Fumu Mussa.