UncategoriesCCM yatekeleza ahadi kwa aslimia 90 Rorya
CCM yatekeleza ahadi kwa aslimia 90 Rorya
Views:
Video Information
Mbunge
wa jimbo la Rorya mkoani mara Lameck Airo amesema utekelezaji wa ahadi
zilizotolewa na chama chamapinduzi (CCM) wakati wa kampeni za uchaguzi
mkuu wa mwaka 2010 umekamilika kwa asilimia tisini katika jimbo hilo.
Akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari jijini Mwanza, Airo amewataka
wananchi wa Rorya kuunga mkono juhudi za kuleta maendeleo zinazofanywa
na serikali na wadau mbalimbali kwa kufanya kazi kwa bidii ili
kufanikisha utekelezaji wa asilimia kumi ya ahadi zilizosalia ikiwemo ya
ujenzi wa barabara ya mika hadi shirati kwa kiwango cha lami kabla ya
juni 2015.