PAULINHO AKIRI ATATUA TOTTENHAM Views: Video Information Kiungo wa kibrazil,Paulinho amekiri kuwa ataiacha klabu yake ya sasa Corinthians na atajiunga na Tottenham ya Uingereza hivi karibuni. Nyota huyo ambaye ameshinda tuzo ya Mpira wa Shaba kama mchezaji bora namba tatu kwenye mashindano ya kombe la mabara akiwa nyuma ya Iniesta na Neymar, anatarajia kujiunga na na klabu hiyo ya London kwa ada ya uhamisho wa pauni milioni 17. Paulinho mwenye umri wa 24 akithibitisha uhamisho huo katika mkutano wa waandishi wa habari - alionekana mwenye masikitiko kuondoka klabu aliyoichezea kwa kipindi kirefu ya Corinthians. Kama uliangalia Confederations Cup - Spurs wamepata ama wamepatikana?