Matangazo

ZILIZO KUPITA HIZI HAPA.

Bongo Flava ni sawa na mtoto anayelelewa na mama peke yake

Mwasyika atimkia Ruvu Shooting

Views:
Video Information
Stephano Mwasyika.
BEKI wa Yanga, Stephano Mwasyika amejiunga na Ruvu Shooting tayari kwa kuichezea timu hiyo ya jeshi.
Chanzo kutoka kwa rafiki wa karibu na beki huyo kilisema Mwasika alijiunga na Ruvu baada ya kuona klabu yake ya Yanga haieleweki juu ya mustakabali wake wa kumsajili.
“Mwasyika baada ya kuona Yanga wapo kimya, ameamua kujiunga na Ruvu na jana (juzi) aliichezea na kuonyesha kiwango cha juu sana,” alisema rafiki huyo ambaye hakutaka kutajwa jina.
Championi Ijumaa lilimtafuta Ofisa Habari wa Ruvu, Masau Bwire ambaye alisema:
“Mwasyika tupo naye lakini bado hatujampa mkataba, amekuja kujaribu bahati yake na tunamuangalia kwa umakini kwanza kabla ya kuchukua maamuzi ya kumsajili moja kwa moja, nafikiri unajua sasa hivi tunahitaji mabeki wawili.
“Kesho ijumaa michuano yetu ya majeshi itaendelea kwa Ruvu kucheza na JKT Mlale na JKT Oljorio itavaana na JKU.
 Source Na Global Publisher
Similar Videos