Matangazo

ZILIZO KUPITA HIZI HAPA.

Bongo Flava ni sawa na mtoto anayelelewa na mama peke yake

Kiggi kupelekwa India mwezi ujao

Views:
Video Information
Kiggi Makasi.
UONGOZI wa Klabu ya Simba ya jijini Dar umeibuka na kusema kuwa mwezi ujao unatarajia kumpeleka nchini India mchezaji wao Kiggi Makasi.
Kiggi amekuwa akisumbuliwa na goti la mguu wa kushoto kwa muda mrefu ambapo amekuwa akirushwarushwa juu ya kupelekwa huko.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema timu ya madaktari wa Klabu ya Simba, ipo katika mchakato wa kusaka ‘appointment’ nchini India ili iweze kumsafirisha mchezaji huyo.
“Timu ya kitabibu ya Simba ipo katika mchakato wa kupata “appointment” nchini India kwa ajili ya kumsafirisha Kiggi ili aweze kupata matibabu nchini humo. Anatarajiwa kwenda mwezi ujao,” alisema Kamwaga.
Similar Videos