Video Information
Mwanzo wa soka unaweza
kupatikana katika kila uwanja wa jiografia
na historia. Wachina, Wajapani, Wakorea na Waitalia wote walikuwa wakicheza
mpira zamani kabla ya enzi zetu. Wagriki na Waromania walitumia michezo hiyo
kuwaandaa wapiganaji kabla ya vita. Hata hivyo, ni nchini Uingereza
ambapo umbo la soka lilianza kuipuka. Ilianza wakati mashirikisho mawili
(Shirikisho la Mpira wa miguu na Mpira wa Ragbi) yalitawanyika. Shirikisho la kwanza lilibakia Uingereza.
Mnamo Oktoba
1963,Vilabu 11 vya London vilituma wawakilishi katika mkutano wa Freemason ili
kijadili na kuweka kanuni zilizokubalika kusimamia mechi zilizochezwa kati yao.
Mkutano huu ulipelekea kuanzisha kwa Shirikisho la Kandanda
(Football Association). Miongoni mwa kanuni zilizowekwa ni zile za kukataa
utumiaji wa mikono kushika mpira na kunyanganya kwa nguvu. Soka na Ragbi
zilitawanyika mnamo tarehe hii. Miaka minane baada ya kuanzishwa, Shirikisho la
Kandanda (FA)
lilikuwa na wanachama 50. Shindano la kwanza la kandanda lilianza mwaka huo- Kombe la FA- ambalo
lilifuatiwa na lile la Ligi ya Ubingwa miaka 17
baadaye. Wachezaji wawili wa Kilabu ya Darwin, John
Dove na Fergus Suter walikuwa
wa kwanza kulipwa kwa mchezo wao. Kitendo hiki kilikuwa mwanzo wa soka ya
kulipwa iliyohalalishwa mnamo mwaka wa 1885. Mwamko huu ulipelekea kuanzishwa
kwa Mashirikisho ya kitaifa nje ya Uingereza (Great Britain). Baada ya Shirikisho
la Kandanda la Uingereza, Mashirikisho yaliyofuatia ni ya Scotland
(1873), Whales (1875) na Ireland
(1880). Kutokana na ushawishi mkuu wa Uingereza katika mataifa ya Dunia, Soka
ilizambaa kote duniani.Mataifa mengi mengine yalianzisha Mashirikisho ya
Kandanda kufikia 1904 wakati Shirikisho la Soka Duniani
(FIFA) lilipoanzishwa.Tangia hapo, kandanda ya kimataifa imekuwa
ikikua licha ya vikwazo mbalimbali. Kufikia 1912, FIFA ilikuwa na uanachama wa Mashirikisho 21, idadi
iliyoongezeka na kufika 36 kufikia 1925. Kufikia 1930- mwaka ambapo kwa mara ya
kwanza kulikuwa na mashindano ya Kombe La Dunia, FIFA ilikuwa na wanachama 41. Idadi hii ilizidi kuongezeka na
kufika 51 mnamo 1938 na 76 kufikia 1950. Baada ya Kongamano la FIFA la mwaka 2000, kulikuwa na wanachama 204 na idadi hii
inazidi kukua kila mwaka.
Kanuni
Maagizo ya Kandanda hupitiwa na
kufanyiwa mabadiliko kila mwaka (Mwezi wa Julai) na Shirikisho la Kandanda Duniani (FIFA).[1]
Mpangilio
wa wachezaji
[2]
[3]
Kuna wachezaji wa aina tatu: Walinzi, wachezaji wa kiungo
na wachezaji wa mbele
au straika. Goli
kipa au mlinda lango ni mmoja
kati ya walinzi. Ni uamuzi wa kocha kuhusu idadi ya wachezaji wanaocheza kuwa walinda lango, wa
kiungo au wa mbele, ikitegemea mfumo uliotumika. Mfumo wa 4-4-2[4]
umekuwa maarufu miongoni mwa timu nyingi. Mfumo huu hujumlisha walinzi wanne
pamoja na mlinda lango, wachezaji wanne wa kiungo na wawili wa mbele.
Utunukizi
wa Alama
Katika ligi za kitaifa na kimataifa,
alama hutunukiwa kwa timu baada ya mchezo. Timu iliyoshinda hupewa alama tatu
huku timu zilizotoka sare hupewa alama moja kila moja. Ikiwa ni lazima mshindi
apatikane, hasa kwenye meji za finali, mchezo huwa na muda wa ziada kama timu
hizo ziko sare. Iwapo sare hiyo huendelea mchezo huamuliwa kwa mikwaju ya penalty.
Shirikisho
la Kandanda Duniani
[5]
Shirikisho la Soka Duniana
(FIFA) ndili shirikisho kuu linalosimamia Kandanda duniani.
Wanachama wake ni mashirikisho ya kandanda ya nchi mbalimbali. Kufikia mwaka wa
2000, lilikuwa na wanachama 204 kutoka pembe zote za dunia. Shirikisho hili
huandaa mashindano mbalimbali ya soka kama vile Kombe la Dunia na pia
huwatunuku wachezaji.
Orodha
ya Wachezaji Maarufu Duniani
[6]
Orodha ifuatayo inaonyesha baadhi ya wanasoka maarufu Duniani, lakini
haiashirii usanjari huu kulingana na ubora. Wapo wengine wengi ambao
hawajatajwa hapa.
- David Beckham wa Uingereza
- Franz Beckenbauer wa Ujerumani
- Gabriel Batistuta wa Arjentina
- Michael Ballack wa Ujerumani
- Pablo Aimar
- Carlos Tevez
- Lionel Messi
- Adriano
- Dennis Bergkamp
- Jared Borgetti wa Mexico
- Fabio Cannavaro
- Roberto Carlos
- Ronaldinho
- Deco
- Hernan Crespo
- Didier Drogba
- Michael Essien wa Ghana
- Samuel Eto wa Cameroon
- Luis Figo
- Steven Gerald
- Thierry Henry wa Ufaransa
- Oliver Kahn, Kipa wa Ujerumani
- Ricardo Kaka
- Roy Keane
- Jurgen Klinsmann
- Miroslav Klose
- Frank Lampard
- Diego Maradona
- Michael Owen
- Alessandro Nesta
- Pele
- Robert Pires
- Rivaldo
- Robinho
- Romario
- Ronaldo wa Brazil
- Cristiano Ronaldo
- Wayne Rooney
- Ruud Van Nistelrooy
- Patrick Viera
- Zinedine Zidane