
Wabunge wa Kiislamu wenye
msimamo mkali nchini Afghanistan wamezuia mjadala wa bunge kuhusu sheria
ya kuwalinda wanawake na dhulma.
Mjadala huo ulikwama baada ya dakika 15 katika
mabishano makali, pale wanasiasa wasiotaka mabadiliko walipotaka sheria
hiyo ifutwe - sheria iliyoanzishwa na Rais Hamid Karzai miaka mine
iliyopita bila ya idhini ya bunge.
Walimshutumu Bw. Karzai kwamba amekiuka sharia za Kiislamu.
Mamia ya watu, hasa wanaume, wamefungwa
kufuatana na sheria hiyo ambayo inapiga marufuku utumiaji nguvu dhidi ya
wanawake, ndoa za watoto na ndoa za lazima.