Matangazo

ZILIZO KUPITA HIZI HAPA.

Bongo Flava ni sawa na mtoto anayelelewa na mama peke yake

BUNGENI NGUMI NJENJE!

Views:
Video Information
Ally Kessy wa Nkasi Kaskazini (kushoto) na Juma Kapuya wa Urambo Magharibi (katikati) baada ya kutibuana.

KUFUATIA baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutibuana katika Mkutano wa 13 wa Kikao cha Bunge la Bajeti 2013/14 kinachoendelea bungeni Dodoma, kuna kila dalili ngumi zikawa njenje, Ijumaa linafunguka.
Tundu Lissu na Anne Kilango wakipandishiana nje ya bunge..
TUNDU LISU Vs ANNE KILANGO
Hayo yameelezwa na wananchi hivi karibuni baada ya Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu na Mbunge wa Same Mashariki (CCM), Anne Kilango Malecela kutibuana nje ya viwanja vya bunge.
Katika tukio hilo, kuliibuka mtafaruku baada ya Kilango kudaiwa kumtuhumu Lissu kwa uchochezi, akidai amekuwa mbunge pekee anayeongoza kwa vurugu mjengoni.
Ilidaiwa kuwa maneno hayo ‘yalimvuruga’ Lissu ambaye alishindwa kuvumilia na kumgeukia Kilango kwa hasira huku baadhi ya wabunge wakishuhudia na wengine wakimzuia na kumtuliza.
Ishu hiyo ilitokea mara baada ya wabunge hao kumaliza kuchangia Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo iliyokuwa na ‘chalenji’ nyingi juu ya kushambuliwa kwa waandishi wa habari.
Ally Kessy akiondoka kwa hasira baada ya kutibuana na Juma Kapuya.
ALLY KESSY Vs JUMA KAPUYA
Katika matukio ya aina hiyo, siku chache kabla ya wabunge hao kutaka ‘kupachimba’, waheshimiwa wengine wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ally Kessy wa Nkasi Kaskazini na Juma Kapuya wa Urambo Magharibi walipandwa na jazba na kutibuana.
Kwa mujibu wa wananchi waliozungumza na Ijumaa wiki hii, kwa sasa ngumi ni njenje hivyo inabidi kila Mtanzania kuliweka bunge hilo kwenye maombi ili limalizike salama kabla hawajatoana manundu ikawa aibu kwa taifa.
  Source:Global Publisher
Similar Videos