Matangazo

ZILIZO KUPITA HIZI HAPA.

Bongo Flava ni sawa na mtoto anayelelewa na mama peke yake

POLISI ARUSHA WAZIDI KUFANYA KAZI ZA SIASA

Views:
Video Information
Hivi ukitazama kwa akili za kawaida tu nini tatizo la jeshi letu la polisi nchini,nini sababu ya kukosa weledi(professi­nalism)kiutendaji?nini kinachosababisha hawa kaka zetu,dada zetu,wadogo zetu na sometimes wazazi wetu hawa kutenda na kufanya
tofauti na tulivyo walea,tofauti na tulivyolelewa natofauti na wanavyyo tulea huko majumbani mwetu kwanini wanakosa adabu na utii kwa watu wengi(wananchi)na kuwa na utii kwa kikundi cha watu wachache(watawala)?nini sababu inayopelekea wao kuwa wauaji,watesaji­,walaRushwa,wab­ambikia kesi ana wasio na huruma na ndugu zao watanzania?Hivi­ UKISHAJIUNGA NA JESHI LA POLISI LA Tanzania UNAKUWA MTU TOFAUTI NA WENGINE,UNAKOSA­ UTU,HESHIMA NA UBINADAMU?SABABU YA HAYA YOTE YANAOFANYWA NA POLISI NI NINI?KWA NINI WANAKUWA SIO WATU WA KULINDA AMANI TENA, BALI KUBOMOA AMANI? TUJIULIZE.TUWAULIZE NA TUULIZANE WATANZANIA TATIZO NI NINI?ELIMU NDOGO,ELIMU KUBWA?,KUTAFUTA­ VYEO ?AMA KUTAFUTA UTAJIRI WA HARAKAHARAKA,?n­auliza tena tatizo ni CCM? ama tatizo ni CHADEMA?je ni kukosa uzalendo?tatizo nini?ama ni hizo bunduki na sare wanazozivaa? hapana mbona hata idala zingine za jeshi wanavaa na kushika bunduki bt hawapo kama hawa polisi?Tatizo wamekubali kutumiwa na watawala ama wanajituma sana?tatzo nini?nauliza wanaipenda sana nchii hii ama wanapenda sana kuogopwa,kwa nini kazi ya siasa wanafanya wao?wajuzi wa sheria hebu mtujuze Polisi anamamlaka gani juu ya raia?mbona hawatulindi raia na mali zetu ?zaidi wamekuwa wanahatarisha usalama wetu na mali zetu?Hebu chukulia mfano wa mbunge wa Arusha mjini GodBless Lema,mtu ambaye jeshi la polisi lilipaswa wampe tunzo kwa kufanikiwa kufanya kazi yao kubwa kwa kuwatuliza wanafunzi wa chuo cha uhasibu Arusha,waliokuwa wamejawa na hasira,jazba na muhemuko wakitaka kuandamana kwenda kwa mtu waliofikiri angekuwa kimbilio lao,angekuwa kipaza Sauti chao kupinga uovu wanaofanyiwa na vijana wasiokuwa na ajira,baada ya kumwua mwenzao na kumpora mali zake,matokeo yake mkuu wa mkoa wa Arusha Magessa Mulongo badala ya kuwatatulia kero zao akawatia uchungu kwa maneno ya jeuri,kiburi cha mbuzi na majivuno ya chatu huku akitoa kauli za kuudhi na dharau ati hawezi kuongea nao bila maiki,ati wasimsogelee sana kwa madai wananuka jasho,hii sio tu haikuwa sawa bali sio haki kwa kiongozi aliye lelewa kwa maadili yote ya kitanzania kuongea lugha hiyo isiyokuwa ya staha na utu kwa binadamu hao wafiwa,Si haki kwa polisi kufanya kazi kwa maagizo ya mkuu wa mkoa hata kama yeye ndo mkuu wa ulinzi na usalama wa mkoa,sio utamaduni wetu kwenda kumkamata kiongozi na mwakilishi wa wananchi milioni zaidi kwwa kumvizia kama kibaka na jambazi sugu,sheria inasemaje kuhusu hilo,sheria ipo wazi kabisa lazima wawe na aresting warrant na searching order na sio kukurupuka kuvamia na kukamata,hivi ndugu zangu polisi mnajiamini nini?ama mnaishi wapi?mbinguni?namshukuru Mungu uzao wetu hakuna damu yetu imejinga na jeshi hili linalofanya maovu kwa asilimia kubwa kuliko mazuri,hata Mungu akija kunijalia watoto sitoruhusu hata mmoja kuwa polisi,kuoa ama kuolewa na polisi ili kuuepusha uzao wetu na sehemu ya uovu,kuanzia leo hata nikumbwe na masaibu gani sitotoa taarifa polisi wala kuhitaji msaada wao,na kwa wale marafiki zangu waliojiunga na polisi hamjachelewa plz msiwe sehemu ya uovu kwa kutenda uovu,fateni kanuni,taratibu na sheria halali za nchi na za jeshi la polisi huku ukimtanguliza HAKI,UTU,HESHIMA na kuitii KATIBA ya Nchi yetu
Similar Videos