Video Information
KAULI YA MKE WA MBUNGEGODBLESS LEMA SASA HIVI KUHUSU
LEMA KUSHIKILIWA POLISI
Taarifa za sasa kutoka Arusha ni
kwamba Mbunge wa Arusha mjini
Godbless Lema anaendelea
kushikiliwa na jeshi la polisi Arusha
na kuhojiwa kwa tuhuma za
uchochezi wa vurugu za Wanafunzi
wa chuo cha Uhasibu dhidi ya Mkuu
wa Mkoa Arusha juzi.
Taarifa za uhakika kutoka kwa mke
wa Mh. Lema sasa hivi ni kwamba
Polisi wamekataa kutoa dhamana
yake na kusema mpaka jumatatu
ndio itajulikana.
Namkariri Mke wa Lema akiongea na
TheTZA millardayo.com akisema
“jana usiku saa sita kasoro watu
walikuja kugonga nyumbani kwetu
tukamtuma kijana aende kutazama
ni kina nani, aliporudi akasema ni
Polisi.. sisi hatukuamini na tulikataa
kwa sababu hatukujua kama ni Polisi
kweli au ni watu wanataka kuitumia
hiyo nafasi kufanya uhalifu, mimi
nimeshinda Polisi kutwa nikifatilia
gari mbona chochote hakikutokea?”
“Baada ya muda kusogea ikabidi
Lema aanze kuwapigia marafiki,
jamaa na baadhi ya viongozi wa
Chadema, kabla ya hapo pia
tuliamua kupiga kengele ya kampuni
ya security ambao muda mfupi
baadae walikuja na gari yao huku
Polisi wakiendelea na vitisho
kwamba watapiga mabomu na
kuvunja ukuta la sivyo Lema
ajisalimishe, Viongozi wa Chadema
na marafiki walipowasili
wakamshauri Lema ndio akajitokeza
wakati huo ni saa tisa usiku” –
Mama Lema
“Alipojitokeza Polisi walimchukua na
mimi nikaondoka nao, tulipofika
kituoni walimtaka Lema kutoa
maelezo lakini alikataa na kusema
mpaka mwanasheria wake aje hivyo
akapelekwa rumande, asubuhi
tulipoamka na kuanza kufatilia..
R.C.O alisema yuko kwenye kikao na
haongei na yeyote isipokua
Mwanasheria wa Lema, walipomaliza
kikao saa nane maelezo yakaanza
kutolewa huku Mwanasheria
akiwepo na kazi ikamalizika jioni saa
11 ambapo Polisi wamekataa kutoa
dhamana mpaka Jumatatu”
– Mama Lema
“shitaka kubwa lililo mbele yake ni
uchochezi na kauli ambayo
anadaiwa Lema kuitoa mbele ya
Wanachuo cha Uhasibu kwamba
dhambi kubwa kuliko zote ni uoga,
na hata leo kwenye maelezo Lema
amewaambia watu wa Arusha mjini
hivyohivyo, kwamba dhambi kubwa
kuliko zote ni uoga” – Mama Lema
Kwa kumalizia, Mke wa Mbunge
Lema amesema “gari letu lililokua
linashikiliwa na Polisi tumerudishiwa
baada ya kutakiwa kulipia elfu 50 ya
wale waliolivuta, gari liko zima
kabisa………… toka nimeolewa na
Lema nimeshuhudia akienda polisi
zaidi ya mara 20, mara yake ya
kwanza kushuhudia anapelekwa
polisi ni wakati wa kampeni za
Ubunge”