Video Information

Aliyekuwa mwigizaji daraja la kwanza katika tasnia ya filamu Tanzania Juma Kilowoko 'Sajuk'i amefariki dunia,
Taarifa kutoka vyombo kadhaa vya habari
ambazo pia zimesibitishwa rasmi na msanii mwingine mkongwe katika tasnia
hiyo Suzane Lewis 'Natasha' zinasema kuwa ‘Sajuki’ amefariki dunia leo
katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, alikokuwa kufuatia tukio la
kudodoka jukwaani jijini Arusha mwishoni mwa mwaka uliopita, wakati
alipokuwa akitoa salamu za shukurani kwa Watanzania kumuombea na
kumchangia kwa hali na mali wakati alipokuwa kwenye matibabu nchini
India.R.I.P SAJUKI DAIMA TUTAKUKUMBUKA.