Matangazo

ZILIZO KUPITA HIZI HAPA.

Bongo Flava ni sawa na mtoto anayelelewa na mama peke yake

Russia yakosoa mshirika wake Syria.

Views:
Video Information
Waziri mkuu wa Russia Dmitry Medvedev.
 
Russia imetoa moja ya ukosoaji wake mkali  dhidi ya rais wa Syria Bashar al- Assad na kusema mshirika wake huyo wa muda mrefu amefanya kosa kubwa kwa kuchelewesha mabadiliko ya kidemokrasia   yanayodaiwa  na upinzani wa Syria.
Waziri mkuu wa Russia Dmitry Medvedev alisema hayo katika mahojiano na televisheni ya CNN  Jumapili . Alisema Bw.Assad  alitakiwa kufanya kazi haraka ili kuzungumza na wapinzani wa mrengo wa kati.
Medvedev  alisema anaamini nafasi ya rais Assad kubaki madarakani inazidi kuwa haififu, lakini akakariri msimamo wa Russia kwamba hatima ya Syria sharti ibaki mikononi mwa raia wa Syria.

Russia imekuwa   ikitoa silaha kwa familia  ya Assad kwa muda mrefu na imepinga maazimio ya baraza la Usalama la Umoja wa  Mataifa yanayotoa mwito kwa jamii ya kimataifa kuingilia kati kuzima mzozo  nchini humo.
Similar Videos