Mabaharia watano wa India
waliotekwa nyara mwezi uliopita nje ya mwambao wa Nigeria wameachiliwa
huru, kwa mujibu wa kampuni yao.
Mabaharia hao wa meli ya mafuta walitekwa wakati
watu waliojihami na silaha tele walipoingia kwa nguvu ndani ya meli
yao, SP Brussels, katika eneo la mafuta la Niger Delta kusini mwa
Nigeria.

Taarifa ya kampuni ya meli hiyo, Medallion
Marine, ilieleza kuwa mabaharia hao ni wazima lakini haikueleza iwapo
ililipa kikombozi.
bbc swahili