Matangazo

ZILIZO KUPITA HIZI HAPA.

Bongo Flava ni sawa na mtoto anayelelewa na mama peke yake

Kundi la al-Shabab latishia kuuwa Wakenya

Views:
Video Information
Wanamgambo wa al-Shabab
                        
Kundi la wanamgambo la  al-Shabab kutoka  Somalia linasema litauwa mateka wao kadhaa raia wa Kenya  ikiwa  Kenya  haitatimiza  madai yao ya kuwaachia waislam waliokamatwa kwa mashitaka ya ugaidi.

Kundi hilo lilitoa vitisho hivyo kwenye Video na kutumia mtandao wa  Twitter  Jumatano usiku . Video hiyo inaonyesha watu 6 wanaosadikiwa kuwa raia wa Kenya wakiwa wameshikiliwa na al-Shabab , wawili kwenye kamera na wanne kwenye picha.


Kwenye mtandao wa Twitter, al-Shabab wamesema watauwa watu hao ikiwa serikali ya  Kenya  haitatimiza madai yao ya  kuwaachia huru waislam wote wanaoshikiliwa kwa mashitaka ya ugaidi nchini humo , na kuachiwa  wengine waliopelekwa nchini Uganda kujibu mashitaka ya ugaidi nchini humo.  Kundi hilo la wanamgambo linasema  linaipa serikali ya Kenya  hadi Februari 14 kujibu madai yake.
Similar Videos