Video Information

Nahodha wa Zambia Chris Katongo
Zambia mabingwa watetezi wana kibarua cha kutetea taji lao walilolipata mwaka jana katika fainali za Kombe la Afrika za mwaka 2012 zilizoandaliwa kwa pamoja kati ya Gabon na Equatorial Guinea.
Kocha mkuu wa Zambia Herve Renard ana kikosi kamili atachochagua kuwavaa Ethiopia katika mechi yao ya ufunguzi ya kundi C.
Zambia inatafuta kuwa moja ya nchi nne zilizoweza kutetea Kombe la Mataifa ya Afrika.
Timu ya Zambia maarufu kama Chipolopolo imechagua wachezaji 19 kati ya wale waliotwaa ubingwa mwaka jana.
Ethiopia wanashiriki kwa mara ya kwanza katika fainali hizo tangu mwaka 1982.

Japokuwa Zambia imepoteza mechi tatu kati ya nne za kujipima nguvu kabla ya michuano hiyo, Renard anaweza kuwaita kwenye kikosi chake Christopher Katongo, mchezaji bora wa mwaka wa BBC, Stoppila Sunzu anayetarajiwa kujiunga na Reading ya England na mlinda mlango Kennedy Mweene.