Matangazo

ZILIZO KUPITA HIZI HAPA.

Bongo Flava ni sawa na mtoto anayelelewa na mama peke yake

JAILUN KUTOA VIDEO YA WIMBO WAKE MPYA

Views:
Video Information
Msanii wa kizazi kipya nchini Tanzania JAILUN  anayetamba na wimbo wa Anakuibia aliomshirikisha Neiba amesema yupo mbioni kuachia video mpya ya wimbo wake unaoitwa Star ambao amemshirikisha Diamond Plutnumz

Jailun ambaye yupo chini ya mameneja wawili ambao ni papaa misifa pamoja na Ngereza

pia Jailun amesema Ngereza ni meneja wake ambae wametoka mbali tangu kipindi Jailun akiwa anaishi Boma Wilaya ya Hai lakini yeye ni mzaliwa wa Arusha na kwa sasa yupo Dar es salaam.

Jailun amesema kuwa Ngereza aliweza kusababisha yeye kurekodi wimbo wa Nalia na wewe ambao aliufanya kwa Mazuu pale Mazuu Records.

 Jailun ameweza kusema juu ya wimbo wake alio mshirikisha Diamond na kusema ilikuwa vigumu kumpata Diamond na kuweza kufanya nae kazi lakini alisema Diamond ni mtu mwelewa na pia wametoka mbali wameweza kufanya show Boma na pale Moshi mkoani Kilimanjaro. Jailun yupo na wenzake Rich Mavocco,Timbulo,Sam Waukweli na Dayna kwa meneja wao Papaa Misifa.

Na Jailun ameweza kusema kuwa mziki wake upo kwenye damu na anahitaji sapoti kutoka kwa wadau ili aweza kuutangaza vema mziki wa Tanzania na amesisitiza kuwa muziki sio uhuni bali ni kazi kama kazi nyingiune


Similar Videos