Video Information

Kambi ya wakimbizi nchini Syria
Shirika la kutoa misaada la International Rescue Committee, limeonya kuwa eneo la Mashariki ya kati linakabiliwa na Janga kuu la kibinadamu kutokana na Vita vya Syria.
Shirika hilo sasa linatoa mwito wa msaada mkubwa zaidi kutolewa na jamii ya kimataifa likisema ule uliotolewa kufikia sasa hautoshelezi kamwe.
Takriban watu millioni mbili wameachwa bila makao nchini Syria.
Shirika hilo linaongezea kuwa masaibu ya ubakaji ni miongoni mwa mambo yanayoandamana na Vita hivyo vya wenyewe kwa wenyewe na ambalo hutekelezwa mbele ya Familia za Waathiriwa.