Matangazo

ZILIZO KUPITA HIZI HAPA.

Bongo Flava ni sawa na mtoto anayelelewa na mama peke yake

Ghasia zaripuka Port Said Misri

Views:
Video Information
maandamano ya Port SaidKumetokea ghasia katika mji wenye bandari wa Misri, Port Said, baada ya mahakama kutoa hukumu ya kifo kwa washtakiwa 21 kuhusu ghasia zilizotokea kwenye mechi mwaka jana.
Watu kama 16 wameuwawa pamoja na askari polisi wawili na wengine kama 50 wameumia.
Ghasia hizo zilianza baada ya wafuasi wa washtakiwa kupambana na polisi nje ya gereza wanamozuwiliwa.
Jeshi sasa limetumwa hapo.
Mwaka jana ghasia kwenye kandanda ziliuwa watu kama 70 baada ya mechi baina ya klabu ya Port Said na ile kutoka Cairo.
Polisi walilaumiwa kuwa hawakufanya kitu kuzuwia fujo hizo za mwaka jana.

bbc swahili
Similar Videos