Video Information

Novak Djokovic akishangilia ubingwa wa Australian Open
Katika mashindano ya Tennis
mchezaji nambari moja duniani Novak Djokovic, leo ameshinda taji la la
nne katika mashindano ya tennis ya Australia Open pale alipomuangusha
Andy Murray, katika fainali.
Mchezaji huyo kutoka Serbia, alitumia muda wa
saa tatu na dakika arobaini kumshinda Murray kwa seti tatu kwa moja za
6-7 7-6 6-3 na 6-2.
Andy Murray akiokoa moja ya mipira
Kufuatia ushindi huo, Djokovic sasa ameshinda mataji sita katika mashindano ya tennis ya Grand slam na kuandikisha historia ya kuwa mtu wa kwanza kuwahi kushinda fainali za mashindano hayo ya Australia kwa miaka mitatu mfululizo, tangu miaka arobaini na sita iliyopita.