Video Information
Chelsea imeweza kupata pointi tatu muhimu katika kinyang'anyiro cha ligi kuu ya England baada ya kuilaza Arsenal magoli 2-1 katika uwanja wa Stanford Bridge.
Juan Mata alipachika bao la kwanza la Chelsea kabla ya Frank Lampard kufunga bao la pili kupitia kwamkwaju wa penalti.
Hata hivyo Arsenal kupitia kwa mshambuliaji wake Theo Walcott aliweza kufunga bao zuri, akiwazidi maarifa walinzi wa Chelsea pamoja na mlinda mlango wao Peter Cech

Huu ni ushindi wa kwanza kwa Chelsea katika uwanja wake mwaka huu 2013 kati ya mechi nne ilizocheza uwanjani hapo Stanford Bridge.